Wakati Wizara mbalimbali zikiendelea kuwasilisha bajeti zao ikiwemo makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2016/2017, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto ambayo may 11 iliwasilisha bajeti yake ambayo imejadiliwa kwa siku mbili mfululizo.
Vipaumbele kadhaa vililengwa ikiwa ni pamoja na hili la kero za wakinamama pindi wanapokwenda kujifungua hospitali, Mbunge wa Nzega Hussein Bashe kaliona na hakutaka kulikalia kimya…
>>’Kwa takwimu tunapoteza wakinamama 42 kwa siku kama nchi, tuitake Wizara ya fedha impatie Waziri wa afya shilingi bilioni 7.5 mwaka huu ili wakinamama wote wakatiwe bima ya afya‘
‘Kwa wastani wakinamama wanaojifungua kwa mwaka ni sawa na kama milioni 1.2, Waziri wa Fedha akatafute fedha hizo popote ili wakinamama hawa nchi nzima wajifungue bila kwenda hospitali na vifaa vya kujifungulia‘
‘Hii itakuwa ni njia moja ya kupunguza vifo vya wakinamama, nasema hivi kwasababu nafahamu ugumu wa maisha ya watu wetu, tumkabidhi Waziri wa Afya hospitali zote za mikoa itatusaidia suala la usimamizi wa Sera, sekta ya afya‘
Unaweza kuendelea kumsikiliza Bashe kwenye hii video hapa chini…
ULIIKOSA HII WIZARA YA AFYA IMEWASILISHA BAJETI YAKE YA BILIONI 845?
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE