Mbunge wa Kuteuliwa, Dkt Bashiru Ali amesimama bungeni leo kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe kuwa Mbunge na kuchangia mjadala wa Wizara ya Kilimo na kuliomba Bunge la 12 kuweka historia kwa kuibadilisha sekta ya kilimo.
“Tujipe ajenda bunge liweze kuwa na mchango wa uhakika wa kubadilisha sekta ya kilimo, bunge la 11 katika historia litatambulika kwa kuleta mabadiliko makubwa sana ya kisera na kisheria kwenye sekta ya madini na tumeona matokeo yake” Bashiru
“Hili la 12 chini ya uongozi wako (Spika Ndugai) na ndani ya serikali chini ya mama Samia tujipe jukumu la kubadili sekta ya kilimo hili sifa hizi mbaya za tija duni, hukosefu wa masoko na kutoyaongezea thamani mazao yetu ya kilimo zibadilike ili tufanane na sekta nyingine zinazobadilika kwa haraka” Bashiru