Millard AyoMillard Ayo
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
  • Contact
Search
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Reading: Bashungwa aja na muarobaini wadaiwa sugu TBA
Share
Notification Show More
Latest News
Waziri Mkuu ashtukia mchezo mchafu Kigoma, ‘zinapotea kinyemela, naleta timu’
September 22, 2023
Waziri wa Michezo, Dkt Damas Ndumbaro ajiuzulu nafasi hii kwenye uongozi wa TFF
September 22, 2023
GSM Home wamekuletea ‘Gulio la Kibabe’, haijawahi tokea wahi sasa, Ommy Dimpoz afunguka
September 22, 2023
Arsenal haihitaji motisha ya ziada dhidi ya Spurs- Arteta
September 22, 2023
Derby ya London Kaskazini huko Arsenal ni ‘changamoto kubwa’ – Postecoglou
September 22, 2023
Aa
Millard AyoMillard Ayo
Aa
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Search
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Follow US
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Millard Ayo > Blog > Top Stories > Bashungwa aja na muarobaini wadaiwa sugu TBA
Top Stories

Bashungwa aja na muarobaini wadaiwa sugu TBA

September 7, 2023
Share
3 Min Read
SHARE

Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa, ameuagiza Wakala wa Majengo (TBA) kuhakikisha unakusanya deni la Shilingi Bilioni 81.5 wanazodai kwa wapangaji wao sambamba na kuwaondoa wadaiwa sugu katika nyumba hizo  ili upatikanaji wa fedha hizo uweze kusaidia utekelezaji wa miradi mingine nchini.

“TBA simamieni sheria kwa yeyote asiyelipa kodi hata kama ni kiongozi, waandikieni notisi ya kulipa madeni yao na wasipolipa waondoeeni, wapo wengine nje wanasubiri wapewe nyumba ili waweze kulipa kodi kwa wakati na tutamia makusanya hayo kujenga nyumba nyingine”, amesisitiza Bashungwa.

Ameyasema hayo leo Septemba 07, 2023 jijini Dodoma wakati Waziri huyo alipofanya ziara yake kwa mara ya kwanza katika Wakala huo na kuzungumza na menejimenti ya TBA ambapo amesisitiza uwekezaji wenye tija kwa watumishi na Taifa kwa ujumla.

Aidha, Bashungwa ameagiza TBA kuhakikisha wanakuja na mikakati itakayosaidia kujenga nyumba za bei nafuu hasa kwa vijana wanaoajiriwa katika utumishi wa umma hususan Dodoma ili kuweza kumudu gharama za maisha.

.

“Kuna vijana ambao wanaingia kwenye kada ya utumishi wa umma na bado hawajawa na uwezo wa kujijengea nyumba, kupitia TBA mnaweza kujenga nyumba za bei rahisi kwa ajili ya vijana hao ili kuwarahisishia gharama za Maisha”, amesema Bashungwa.

Kadhalika, Bashungwa ameutaka Wakala huo kuwa na utaratibu wa kuwajengea uwezo wataalamu walionao ili kuenda sambamba na kasi ya mabadiliko ya teknolojia hasa katika suala la ujenzi na uendelezaji wa majengo mbalimbali.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa TBA, Arch. Daud Kondoro, amesema kuwa Wakala huo utahakikisha unatafuta ufumbuzi wa changamoto zilizopo na kumuahidi Waziri Bashungwa kuandaa mikakati mizuri itakayosaidia Wakala huo kutoa huduma bora kwa wananchi.

.

Awali, Arch. Kondoro ameeleza kuwa hadi sasa TBA inaendelea kutekeleza mradi wa ujenzi wa nyumba 3500 za watumishi wa umma eneo la Nzuguni Dodoma ambapo awamu ya kwanza ya nyumba 150 utekelezaji umefikia asilimia 95 na awamu ya pili ya ujenzi wa nyumba 150 utekelezaji wake umefikia asilimia 10.

Miradi mingine ni ujenzi wa nyumba 20 za Viongozi jijini Dodoma ambazo zililenga kukabiliana na uhaba wa nyumba za Viongozi baada ya Serikali kuhamia Dodoma ambapo mradi huo umekamilika kwa asilimia 100 na nyumba zimeanza kutumiwa na Viongozi.

Waziri Bashungwa anaendelea na ziara yake ya kutemebelea Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi ambapo leo ametembelea na kuzungumza na menejimenti ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).

 

You Might Also Like

Waziri Mkuu ashtukia mchezo mchafu Kigoma, ‘zinapotea kinyemela, naleta timu’

Waziri wa Michezo, Dkt Damas Ndumbaro ajiuzulu nafasi hii kwenye uongozi wa TFF

GSM Home wamekuletea ‘Gulio la Kibabe’, haijawahi tokea wahi sasa, Ommy Dimpoz afunguka

Kuelekea fainali ya polisi jamii DPA cup mashabiki wajigamba afisa michezo atoa neno

Nigeria:Tinubu aidhinisha nyongeza ya mishahara kwa Taasisi za Elimu ya Juu za Shirikisho

Edwin TZA September 7, 2023
Share this Article
Facebook TwitterEmail Print
Share
Previous Article Mradi wa hewa ukaa mbioni kuanzishwa Kigoma
Next Article Mtanzania Alice Gyunda yupo TOP 20 ya Wanaowania Miss/Mrs Africa Uingereza
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

You must be logged in to post a comment.

- Advertisement -

Latest News

Waziri Mkuu ashtukia mchezo mchafu Kigoma, ‘zinapotea kinyemela, naleta timu’
Top Stories September 22, 2023
Waziri wa Michezo, Dkt Damas Ndumbaro ajiuzulu nafasi hii kwenye uongozi wa TFF
Top Stories September 22, 2023
GSM Home wamekuletea ‘Gulio la Kibabe’, haijawahi tokea wahi sasa, Ommy Dimpoz afunguka
Top Stories September 22, 2023
Arsenal haihitaji motisha ya ziada dhidi ya Spurs- Arteta
Sports September 22, 2023

You Might also Like

Sports

Derby ya London Kaskazini huko Arsenal ni ‘changamoto kubwa’ – Postecoglou

September 22, 2023
Sports

Xavi kuongeza mkataba wa Barcelona hadi 2025

September 22, 2023
Top Stories

Kuelekea fainali ya polisi jamii DPA cup mashabiki wajigamba afisa michezo atoa neno

September 22, 2023
Top Stories

UN yaitaka Iran kuachana na sheria mpya kuhusu hijab

September 22, 2023
Show More
//

To be recognized as Africa’s leading and most trusted online media network providing quality content across all our media platforms by 2025

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

Millard AyoMillard Ayo
Follow US

© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.

Removed from reading list

Undo

Lost your password?