Top Stories

Bashungwa ataoa onyo watumiaji mitandao “matusi hapana” (+picha

on

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa ameonya watumiaji wa mitandao ya kijamii kinyume na Kanuni ya Maudhui Mtandaoni za 2018 ambazo zinawazuia watumiaji wa mitandao hiyo kutokutumia lugha za kuudhi/matusi na kutokusambaza taarifa za uongo au za upotoshaji.

Waziri Bashungwa amesema hayo leo jijini Arusha wakati wa kongamano la fursa kwa wanamuziki lililoandaliwa na Taasisi ya kijamii inayoshughulika na wanamuziki (TAMUFO) ambalo jukumu lake ni kuhamasisha maendeleo, kupambana na umaskini, ujinga na maradhi na kuwa na usawa katika mgawanyo wa mapato yanayotokana na muziki kwa wanamuziki.

Ikumbukwe Julai 17, 2020, Serikali ilichapisha mabadiliko ya Kanuni za Maudhui Mtandaoni kwenye gazeti la Serikali kupitia gazeti Na.29 Toleo la 101 ambayo yalitolewa kupitia notisi Na. 538 yanabadilisha baadhi ya Kanuni za Maudhui Mtandaoni za mwaka 2018 ili kuhakikisha zinalinda maslahi ya watumiaji wa mitandao hiyo bila kuleta taharuki zisizo za lazima katika jamii.

Aidha, Waziri Bashungwa amewataka Watanzania kuendelea kuliombea taifa hatua itakayowasaidia wananchi kuendelea kuwa na afya bora ili kupambana dhidi ya magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza.

Akiongea na wasanii pamoja na wadau waliohudhuria kongamano hilo, Waziri Bashungwa amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha kila msanii ananufaika na kazi yake pamoja na kuongeza pato la taifa.

“Nimetoa maelekezo kwa Chama Haki Miliki (COSOTA) wakamilishe mfumo utakaosaidia kutambua kazi za wasanii zinapotumika kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wahakikishe kila redio, TV, mabasi, baa ama kumbi za starehe ambao utatambua na kusaidia kukusanya mapato ambayo yatrasaidia wananamuziki kunufaika na kazi zao,” Waziri Bashungwa.

MTANZANIA AUNDA MAGARI, CROWN ATHLETE IPO, ANAPIGA HELA “WAZUNGU WANANUNUA”

Soma na hizi

Tupia Comments