Habari za Mastaa

Aliemtetea Michael Jackson ahamia kwa R Kelly

on

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umeripoti kuwa Mwanasheria aliyewahi kusimamia kesi ya kulawiti watoto wadogo iliyokuwa ikimkabili Marehemu Michael Jackson mwaka 2005 na kushinda kesi hiyo sasa atajiunga kwenye kundi la Wanasheria watakomtetea mwimbaji R Kelly.

Inaripotiwa kuwa Mwanasheria huyo anayejulikana kwa jina la Thomas Mesereau alikutana na R Kelly  jijini Chicago kwa ajili ya kufanya mazungumzo juu ya mashtaka zaidi ya 12 ya unyanyasaji wa kingono kwa wasichana wadogo ambayo bado yanamkabili mkongwe huyo wa muziki. Iliripotiwa kuwa July 16,2019  R Kelly alinyimwa dhamana baada ya kukana mashtaka yote yanayomuandama akiwa chini ya Mwanasheria Nicole Blank Becker.

June 6,2016 R. Kelly alipandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Cookmjini Chicago ili kujibu mashtaka yote 11 ambapo makosa manne yalitajwa kupewa daraja X na kuwekwa kwenye kipengele cha makosa ya jinai, imeripotiwa kuwa Thomas Mesereau aliwahi kuwa Mwanasheria wa Mchekeshaji Bill Cosby kwenye kesi  iliyokua ikimuandama ya unyanyasaji wa kingono mwaka 2004

VIDEO: ROSE NDAUKA KUHUSU KUTENGANA NA MZAZI MWENZAKE ‘NILICHOKA KILA MTU ATAVUNA ALICHOPANDA” BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA.

Soma na hizi

Tupia Comments