Michezo

Hatimae Ligi Kuu Tanzania bara imepata mdhamini

on

Baada ya Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2018/2019 kuchezwa bila uwepo wa mdhamini mkuu kiasi cha kupelekea baadhi ya mambo kukwama ikiwemo tuzo za wachezaji.

Leo hii shirikisho la soka Tanzania TFF limetangaza rasmi kupata mdhamini wa Ligi hiyo kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom ambao walikuwa wadhamini wa kuu kwa miaka kadhaa.

TFF na Vodacom wameingia mkataba wa miaka mitatu wa kudhamini Ligi Kuu, mkataba ambao una thamani ya Tsh Bilioni 9 ambapo kila mwaka katika kipindi cha miaka mitatu itakuwa ni Tsh Bilioni 3.

Soma na hizi

Tupia Comments