Habari za Mastaa

Jay Z atajwa na na Jarida la Forbes kuwa ndie msanii wa Hip Hop tajiri zaidi

on

Kwa mujibu wa jarida la Forbes limemtaja rapper Jay Z kama msanii wa kwanza kwenye game ya muziki wa Hip Hop kufikia utajiri wa Dola Bilioni moja za Kimarekani sawa na zaidi ya shilingi Trilioni 2 za Kitanzania.

Katika toleo jipya la Jarida hilo limemtaja Jay Z kufikisha utajiri huo kutokana na biashara zake ikiwemo ndani na nje ya muziki ikiwemo kampuni ya Roc Nation, gharama kubwa ya nyumba anazomiliki, Catalog za muziki na vitu vingine mbalimbali.

Mwaka 2018 jarida la Forbes lilimtaja Jay Z kushika nafasi ya 5 akiwa alichuana na Kylie Jenner kwa kuwa na utajiri wa kiasi cha dola Milioni 900 sawa na zaidi ya shillingi Trillion 2 za Kitanzania.

VIDEO: ULIPITWA NA HII YA STEVE NYERERE AKIPAKUA FUTARI KWA MAKONDA? BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA

Soma na hizi

Tupia Comments