Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara limewafikisha Mahakamani Viongozi wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) Mkoa wa Manyara kwa kosa la kufanya mkutano wa hadhara bila kuwa na kibali.
Akithibitisha kukamatwa na kufikishwa Mahakamani kwa Viongozi hao RPC wa Manyara ACP Benjamin Kuzaga amesema Viongozi hao wamekamatwa mnano tarehe 15/01/2022 katika maeneo ya Kateshi Stand, Wilaya ya Hanang, Manyara.
Kuzaga amewataja viongozi hao waliokamatwa kuwa ni Ngigula Rafael 45) Mwenyekiti wa BAWACHA Manyara, Valentina Shayo (37) Mhasibu BAWACHA na Tasira Karama, Mjumbe wa Kamati Tendaji BAWACHA Manyara.
Polisi wamesema Wahumiwa hao wamekamatwa kwa kufanya mkutano wa hadhara bila kuwa na kibali na baada ya kuhojiwa na Polisi walikiri kufanya kosa hilo la kufanya mkutano bila kuwa na kibali na baada ya Polisi kukamilisha upelelezi 17/01/2022 walifikishwa Makamani, shauri hilo limepangwa kuendelea tena Mahakamani tarehe 16/02/2022 kwa hatua ya usikilizaji wa awali, ambapo Polisi Mkoa wa Manyara imetoa wito kwa Wakazi wa Manyara na Vyama vya Siasa kufuata taratibu za ufanyaji wa mikutano kwa kuwa na kibali kutoka mamlaka zinazohusika.
l