Habari za Mastaa

Wasanii kutokea Afrika wahusika kwenye Album mpya ya Beyonce (+Video)

on

Inaripotiwa kuwa muandaaji (Producer) wa ngoma zitakazotumika kwenye filamu ya The Lion King itakayoachiwa rasmi July 17,2019 ni mwimbaji mkongwe Beyonce ambaye tayari ameshatayrisha nyimbo hizo zikiwa zimeshirikisha wasanii tofauti tofauti duniani.

 Fahamu pia kuwa Album hiyo  itahusisha ngoma ambazo zimeandikwa na waimbaji kutokea Afrika huku jina la Album hiyo likiwa  “The Lion King The Gift ” na kutajwa kuachiwa July 19,2019 huku ngoma ya ‘Spirit’ ikiwa tayari imeachiwa kutoka kwenye album hiyo album hiyo imetumia vionjo vya miziki mbalimbali ikiwemo R&B, pop, Hip hop na Afro Beat.

Filamu ya ‘The Lion King’ imehusisha waigizaji kama Beyonce(Nala) , Donald Glover, John Oliver, Seth Rogen na wengine wengi pia iko chini ya watayarishaji  kama Karen Gilchrist, Jon Favreau na Jeffrey Silver

VIDEO: AUNT EZEKIEL, SHILOLE, SHAMSA FORD, WAFUNGUKA KUHUSU SWAHILIFLIX MTANDAO UTAKAOUZA KAZI ZAO

Soma na hizi

Tupia Comments