Habari za Mastaa

Video za Tekashi 69 kutumika kwenye uchunguzi juu ya kesi yake

on

Baada ya Mwanasheria Alex Spiro kuongezeka kwenye orodha ya wanasheria ambao watamsimamia Rapper Tekashi kwenye kesi yake inayomkabili ya kujihusisah na upangaji wa matukio ya kihuni pamoja na kumiliki silaha kinyume na sheria.

Sasa kwa mujibu wa mtandao wa Page Six umeripoti kuwa ikiwa bado Tekashi 69 akisubiri kupandishwa kizimbani September 4,2019, imeeleza kuwa waendesha mashtaka watatumia video zake kwa ajili ya kupata ukweli juu ya kesi inayomkabili huku wakiamini kuwa video hizo zitawafanya kubaini matukio ya kihalifu pamoja na maneno makali yaliyotumika kwenye nyimbo zake kama yana uhalisia na mashtaka yanayomkabili.

Inaelezwa kuwa Tekashi atapandishwa kizimbani kusikiliza kesi yake September 4,2019ambapo tokea November 18,2018 alikua akishikiliwa na kusota kwenye jela ya kijasusi nchini Marekani.

AUDIO: ‘YESU’ FEKI ALIETAMBA KENYA AFARIKI, WACHUNGAJI WAKAMATWA

Soma na hizi

Tupia Comments