Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Baada ya siku 14 rumande Asap Rocky ashtakiwa kwa kosa la kupigana

on

Inaripotiwa kuwa Mahakama ya Sweden imemshtaki rapper Asap Rocky kwa kosa la kumpiga na kumuumiza shabiki mmoja katikati ya mji wa Stockholm June 30,2019, hii ni baada ya rapper huyo kusota rumande kwa takribani wiki mbili sasa.

Baada ya Kim Kardashian, Snoop Dogg kupaza sauti kuhusu kesi hiyo imezidi kuelezwa kuwa Asap Rocky atapandishwa kizimbani wiki ijayo kwa ajili ya kusikiliza kesi yake na imeelezwa kuwa endapo atakutwa na hatia atahukumiwa kifungo cha miaka miwili jela lakini kwa upande wa Asap amezidi kujitetea kuwa kilichotokea ni kujilinda dhidi ya kijana yule.

Siku kadhaa zilizopita Rais Trump alitangaza kumsaidia Asap juu ya kesi yake lakini kumeonekana kutokua na hatua yoyote ambayo ni nzuri hata hivyo mama mzazi wa Asap alisema kuwa Mahakama ya Sweden haifanyi sawa kwa mwanae huku akitaja sababu kubwa ni ubaguzi wa rangi ndio unamfanya mwanae akae rumande.

VIDEO: MREMBO ANAEPIGA VITA KUJICHUBUA “UNAWEZA PATA KANSA HATA YA KIZAZI”

Soma na hizi

Tupia Comments