Habari za Mastaa

Hawa ndio washiriki wengine waliotoka Big Brother….

on

bba-hotshotsMatumaini ambayo wengi wetu tulikuwa nayo kumuona mshiriki wa kutoka Afrika Mashariki ndani ya jumba la Big Brother Africa kuibuka na ushindi, yameshuka kwa kiasi kikubwa baada ya washiriki kutoka nchi mbili za Afrika Mashariki kutolewa nje ya jumba hilo.

Wiki moja baada ya washiriki Lillian kutoka Nigeria, Esther kutoka Uganda na Sabina kutoka Kenya kutolewa kwenye mjengo huo, Mtanzania Laveda aliyekuwa na mahusiano ya karibu na Permithias pamoja na Mkenya Alusa wamekutana na ‘rungu’ la kura lililowatupa nje ya jumba hilo.

BBA Mpya

Laveda anakuwa mshiriki wa 6 wa jinsia ya kike kutolewa nje ya jumba la BBA huku Alusa akiwa ni mshiriki wa kwanza wa kiume kutolewa #BBAHotshots.

Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

 

Tupia Comments