Habari za Mastaa

Kuhusu zile milioni mbili za @bballkitaa Feb7 na pichaz zake. cc @IamNchaKALIH

By

on

24Baada ya kuwa zimetembea Status nyingi facebook, post za Instagram na twitter kuhusu hii ya kugombania milioni mbili February 07 2014, hatimae utata umekatika  baada ya Team Next level ya Adam Juma kushinda milioni mbili zilizowekwa mezani kumtafuta mkali wa mechi hii ya mpira wa kikapu.

1Mchezo huu ulihusisha mechi za waongozaji wa video toka Bongo ambao ni Adam Juma na Karabani kila upande uliweka Milion Moja Cash mezani.

23Mpaka filimbi ya mwisho Team Next Level ya Adam ilichukua Milion Mbili kwa kupiga vikapu 81 kwa 74 kwenye game ambayo ilihudhuriwa na mastaa kibao akiwemo Diamond Platnumz, Queen Darlin, Shettah, Godzilla, Marco Chali, Adam Mchomvu, Salama Jabir, Young Killer, Young Dee, Country Boy, Linex, Navy kenzo, Vanessa V Money na wengine.

19Kadri siku zinavyozidi kwenda BBALL KITAA watu wanazidi kuielewa, pamoja na kwamba ni game inapigwa lakini wengine wanaichukulia kama sehemu ya kutokea, kukutana, kuenjoy na washkaji, ndugu, wapenzi na watu wengine yani ‘outing’ flani hivi pembeni ya bahari, game inachezwa, mziki kwenye spika, vinywaji na msosi wa hapa na pale.

Huu ni ubunifu wa vijana wachache wa Kitanzania walioamua kuleta kitu ambacho hakijawahi kuwepo au kufanyika kwa Watanzania… hivyo support yako pia itahesabiwa… wafate kwenye twitter na instagram kwa jina la >>> @bballkitaa

25

21

2

8

31

diamond

 

27

adam

v

nahreal

Tupia Comments