Habari za Mastaa

AUDIO: Alichokizungumza Baby J kuhusu ndoa yake

on

April 21, 2017 staa wa Bongofleva kutoka Visiwani Zanzibar, Baby J amemzungumzia kuhusu issue ya ndoa yake ambayo ilikuwa gumzo sana baada ya kufunga ndoa saa 11 alfajiri lakini haonekani akiishi na mume wake.

Akijibu swali la mtangazaji wa Leo Tena ya Clouds FM kuhusu ndoa hiyo ambayo baada ya kufunga na mwanaume aliyekuwa anaishi nje ya nchi na yeye kuendelea kuishi Zanzibar, Baby J alijibu:>>>”Wakati najiandaa kusafiri kwenda New York aliko ambako tulipanga mimi na yeye tukaishi, ilitakiwa iwe siku ya 15. Lakini ilipofika siku ya 10 mwenzangu akakamatwa huko aliko. Japo aliniambia kuwa atakamatwa, sijajua nini kilisababisha.

“Wakati anakamatwa ilikuwa saa 10 jioni baada ya muda ule sikumpata tena kwenye simu. Halafu bahati mbaya, mama yake mume wangua alikuwa amakuja Afrika kwa ajili ya harusi, so, nilikuwa niko naye. Bahati mbaya akafariki kwa mshtuko mida ya kama saa 12, na baada ya siku ya pili ndio akanipigia kujua juu ya msiba wa mama yake. Hivi na yeye alikuwa jela ikawa mtihani.

“Tunawasiliana kwa sasa hivi, ila ni mwaka wa tano toka ameshikiliwa. Halafu kipindi mwenzangu anakamatwa, mimi nipo kwenye msiba. Watu wakaanza kunitumia sms wakinisema kuwa tulikuambia, tutaendelea kupishana hapa hapa. Bahati nzuri, mwenzangua alikuwa ameniachia ujauzito mchanga, lakini bahati mbaya uliharibika kutokana na hiyo hali.

“Ninavyowasiliana na mwenzangu, ananisihi sana nivumilie. Nina matumaini japo sitaki kulizungumzia hilo.” – Baby J.

Bonyeza Play hapa chini kusikiliza full story nimekuwekea…

VIDEO: Kinachoendelea shindano la Mr. Tanzania 2017

Soma na hizi

Tupia Comments