Habari za Mastaa

Maneno ya kwanza ya Belle 9 tangu kufiwa na baba yake

on

Leo May 4, 2017 kupitia XXL ya Clouds FM staa wa muziki wa Bongofleva Belle 9 amezungumza kwa mara ya kwanza baada ya msiba huo wa baba yake mzazi akisema kuwa maisha yake kwa sasa yamebadilika.

Usiku wa kuamkia April 18, 2017 zilitangazwa taarifa za kifo cha mzee Damian Nyamoga ambaye ni baba mzazi wa Belle 9 aliyefariki akiwa hospitali akipatiwa matibabu baada ya kugongwa na pikipiki mjini Morogoro.

“Maisha yamebadilika. Zamani nilikuwa nikiongea na mama, ananiambia baba yako huyu hapa ongea naye. Najifunza sasa kuishi maisha mapya. Hii dunia tunapita tu cha muhimu kujiandaa.”

Aidha, Belle 9 amesema anaendelea na maisha yake mengine ambapo ameweka wazi ujio wa video mpya huku akitoa shukrani kwa watanzania wote ambao walikuwa naye katika kipindi chote cha majonzi.

“Tupo location tunafanya video, lakini nimesimamisha kwanza kwa sababu ya kutoa shukrani kwenu na watanzania waliokuwa pamoja nami.

“Now naendelea na maisha yangu. Kelvin Bosco amenipa zawadi ya video kama pole kwangu na hii ngoma haikuwa kwenye plan. So sio vibaya tukiendelea kuhifadhi kwenye maktaba mpaka pale tutakapopata muda wa kuitoa.” – Belle 9.

‘Mimi sio shabiki wa muziki wa Vanessa Mdee ila’– Afande Sele

Soma na hizi

Tupia Comments