Michezo

Staa huyu aliyestaafu soka ametajwa kupewa tuzo maalum ya heshima Uingereza..

on

bekMkongwe wa soka duniani David Beckham amedhihirisha kuwa alitumia vyema nafasi yake akiwa uwanjani na kujenga jina na heshima kwenye soka ambayo itamfanya akumbukwe duniani.

Beckham ambaye alizichezea klabu kama Manchester United na Real Madrid leo kuna headline inamhusu, ukongwe wake na heshima aliyoiacha kwenye soka inafanya watu wanaoandaa event ya HMV Football Extravaganza Uingereza kumtaja kwamba kwenye sherehe hiyo mwaka huu itatolewa tuzo hiyo rasmi kwa David Beckham.

Tuzo hii ni ishara ya kuutambua mchango wa Beckham kwenye soka duniani.

Hata hivyo Beckham mwenyewe ameipokea kwa furaha taarifa hii kwa kuwa kwenye list ya ya wachache waliobahatika kupewa tuzo hiyo ikiwemo Sir Alex Fergusson na Kocha Jose Mourinho.

I’m incredibly honoured to be receiving this award, when you look at the list of the previous recipients, I feel very fortunate to be considered alongside them. ‘More importantly the night is about recognising the fantastic work that Nordoff Robbins does and raising funds for their vital work,“– David Beckham.

Maazimisho ya miaka 20 ya Tuzo za HMV Football Extravaganza yatafanyika September 1 mwaka huu ambapo Beckham atakabidhiwa tuzo yake pamoja na kufanyika harambee ya kuchangisha pesa ambazo zitakwenda kwenye taasisi ya Nordoff Robbins kwa ajili ya kusaidia watu wenye matatizo mbalimbali ya kiafya na kijamii Uingereza.

Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments