Michezo

David Beckham kamshauri Memphis Depay wa Man United kuhusu jezi namba 7

on

Katika soka baadhi ya namba za jezi uwanjani huwa zinaheshimika kubwa uwanjani na wakati mwingine unaweza kukuta klabu wameiweka jezi pembeni kwa sababu hawaoni nani ataitendea haki na kulinda heshima yake. Jezi namba 7 ni miongoni mwa jezi zenye heshima kubwa katika klabu ya Manchester United na moja kati ya watu walioipatia heshima jezi hiyo ni David Beckham na Cristiano Ronaldo.

memphis-depay-manchester-united-goal-celeb-champions-league-kiss-club-brugge_3339233

Memphis Depay aliyesajiliwa msimu huu na klabu ya Manchester United akitokea klabu ya PSV Endhoven ya Uholanzi kwa dau la pound milioni 25 anavaa jezi hiyo kwa sasa. Depay ambaye kwa wiki za karibuni amekuwa akikaa benchi na Jesse Lingard kuchukua nafasi yake, amekuwa akitajwa kuwa na presha kubwa kutokana na wengi kutaka kuona anaifanyia makubwa jezi namba 7 kama walivyofanya Cristiano Ronaldo na David Beckham.

Baada ya maneno mengi kuongelewa juu ya jezi namba 7 David Beckham amempa ushauri Memphis Depay  kuwa hatakiwi kuwa na presha au kuogopa kuvaa jezi hiyo licha ya kuwa inatajwa kuwa na mafanikio makubwa Man United lakini ni heshima kwake kuvaa jezi namba saba.

David_Beckham

David Beckham

“Sioni kama jezi namba 7 inatisha au kuogopesha chochote mimi nafikiria ni heshima kuivaa, unapopewa jezi namba 7 haina maana ya kwamba hadi uwe umeshinda au huyo mchezaji awe amepata mafanikio sana, lakini mwisho wa siku ni jezi maalum kuivaa ila sifikirii kama inakuwa na presha kuivaa binafsi ni jezi inayonihamasisha uwanjani” >>> Beckham 

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FBInstagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments