Habari za Mastaa

Jibu la Mwimbaji Emmanuel Mbasha kuhusu kurudiana na Flora Mbasha

on

Kama utakuwa unakumbuka mnamo September 21,2015 moja ya stori kubwa iliyogusa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania ni ishu ya Hukumu ya Kesi ya Mwimbaji wa Gospel Tanzania, Emmanuel Mbasha ambapo alikuwa anakabiliwa na Kesi ya kumbaka shemeji yake na kesi imekuwa Mahakamani tangu 2014.

Wengi tunafahamu kwamba mwimbaji huyo aliachiwa huru baada ya Mahakama kumkuta hana hatia kwenye Kesi hiyo, sasa leo kajibu swali kuhusu kurudiana na mkewe Flora Mbasha na kuyaongea haya>>

‘Mimi kurudiana na Flora Mbasha ni ngumu kwasababu yeye ndio aliniacha mimi na yeye ndio aliandaa mazingira yake ya kuniacha mimi mpaka ikafika wakati Familia yangu, viongozi mbalimbali wa Dini wakawa wanamshauri lakini akutaka kurudiana na mimi kwahiyo naweza sema ni ngumu kurudiana na Flora’

ULIIKOSA HII YA NAY WA MITEGO KUMALIZANA NA BASATA BASI ITAZAME HII VIDEO HAPA

Soma na hizi

Tupia Comments