Mamlaka ya udhibiti wa usafiri nchi kavu LATRA wametangaza bei mpya za nauli za Mabasi na Daladala nchini ambazo zitaanza kutumika baada ya siku 14 kuanzia leo kutangazwa.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, Gilliard Ngewe amesema nauli za daladala kuanzia km 0-10 nauli itakua shilingi 500 kutoka shilingi 400na km 11-15 nauli itakua shilingi 550 kutoka Shilingi 450 na bei ya mwisho ya daladala kwa km 36 hadi 40 itakua shilingi 1100 kwa daladala tu.
Huku nauli za mabasi yaendayo mikoani zikipanda kwa daraja la kawaida ni shilingi 41.29 kwa kilometer moja kutoka shilingi 36.89 huku daraja la kati ikipanda kwa shilingi 56.88 kutoka shilingi 53.22
Huku nauli kwa wanafunzi ikibakia kua shilingi 200 kwa daladala.
MBUNGE MUSUKUMA AMTAKA WAZIRI AMSIKILIZE “NAONA KAMA TUMEWAINGIZA CHAKA,TUWEKEE MSIMAMO”