Mix

Haya mengine ya kichanga kukutwa hai ndani ya shimo la choo yamenifikia!

on

baby

Stori za kukuta watoto wametupwa chooni hazipo Africa tu bali hata kwa wenzetu pia. Nimekutana na hii moja kutoka Beijing China ambako polisi wameokoa mtoto mchanga aliyetupwa chooni siku chache zilizopita.

Ilikuwa weekend nyingine tu ya kawaida siku ya jumapili jijini Beijing mpaka pale wapita njia walipoanza kusikia sauti ya mtoto mchanga ikitoka kwenye choo cha umma.

china2

Watu waliokuwa wakipita sehemu hiyo walisema kuwa walisikia sauti ya mtoto ikitoka chooni humo na walipoingia walikuta kichwa cha mtoto huyo kipo ndani ya tundu la choo huku mwili wake ukiwa unachungulia juu ya choo hicho.

Baada ya polisi kufika endeo hilo walishindwa kukitoa kichwa cha mtoto huyo kwenye  shimo la choo na kama wangelazimisha kwa kumvuta basi wangemuua mtoto na ili kuokoa maisha ya mtoto huyo ilibidi wakibomoe choo hicho.

china

Juhudi za kumpata mzazi wa mtoto huyo bado zinaendelea kufanyika na polisi wa Beijing.

 PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments