Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na serikali mapema wiki hii, idadi ya wakazi wa Beijing imeshuka kwa 43,000 hadi kufikia watu milioni 21.84 kufikia mwishoni wa mwaka jana.
Ripoti hiyo kutoka mamlaka za manispaa ya Beijing inasema kwamba idadi ya vifo mjini humo imepanda mara 5.72 kwa kila watu 1,000 wakati idadi ya watoto wanaozaliwa ikishuka kwa mara 5.57 kwa kila watu 1,000.
Ongezeko asilia la watu mji humo limekuwa 0.05 chini ya sifuri ikiwa mara ya mwisho kwa idadi ya watu kupungua tangu 2003.
Idadi ya watu mjini Beijing pamoja na miji mingine mikubwa ya China kwa kawaida huhesabiwa kulingana na wakazi wa kudumu na wala siyo wahamiaji.
Hivyo takwimu rasmi za serikali zinaonyesha kwamba Idadi ya watu kwenye mji mkuu wa China, Beijing imeshuka kwa mara ya kwanza ndani ya miongo miwili, ukionekana kuwa mwendelezo wa hali katika maeneo mengine ya taifa hilo ambapo idadi ya watu imeendelea kushuka.