Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imesema watu 10 wamefikishwa Mahakamani katika miezi ya hivi karibuni kwa mashtaka yanayohusiana na noti bandia.
Imesema watuhumiwa wametokea Dar, Mwanza, Arusha, Moshi na Mbeya na operesheni hiyo bado inaendelea na aadhi walikutwa na noti feki na wengine walikutwa na mashine zinazotumika kuzitengeneza.
Benki Kuu imeeleza wasiwasi wake kuhusu wahalifu kulenga minada ya mifugo na mazao ili kutoa fedha hizo kwa wakulima na wafugaji ambao hawazitambua.
Desemba mwaka jana, Gavana Florens Luoga alihimiza adhabu kali kutolewa kwa watakaokutwa na hatia na kutengeneza na kusambaza noti bandia