Michezo

Benzema ahukumiwa mwaka mmoja jela

on

Mshambuliaji wa Real Madrid na Timu ya Taifa ya Ufaransa Karim Benzema amehukumiwa mwaka mmoja jela na faini ya euro 75000 (Tsh milioni 194).

Hukumu hiyo imetoka baada ya kosa hilo kutokea 2015 ambapo Benzema inadaiwa kuwa alishirikiana na watu wasiojulikana kumlaghai mchezaji mwenza wa Ufaransa Mathieu Valbuena atoe pesa kuwalipa watu hao ili wasitoe video yake ya ngono.

Hata hivyo baada ya hukumu hiyo kutoka na Benzema kukutwa na hatia hatotumikia kifungo jela ila atakwenda jela endapo atafanya kosa jingine hivi karibuni ndio adhabu yake ataenda kuitumikia jela.

Soma na hizi

Tupia Comments