Michezo

Alichokisema Arsene Wenger kuhusu Karim Benzema nimekuwekea hapa

on

article-2681864-1F6B640000000578-973_634x639

Wiki kadhaa sasa zimepita toka uvumi kuhusiana na mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa anaeichezea klabu ya Real Madrid ya Hispania Karim Benzema kuuhusishwa kujiunga na Arsenal. Wengi wanaamini Benzema atahamia Arsenal kutokana na Wenger kuwa na utamaduni wa kupenda wachezaji kutokea Ufaransa.

Karim+Benzema+Marcelo+Real+Madrid+v+Malaga+hhDRUO1Wc-fl

Mwezi uliopita mkurugenzi wa Arsenal Lord Harris alisema Wenger tayari ana jina la mshambuliaji wa kati anayetaka kumleta Emirates msimu huu ambapo watu walihisi atakuwa Karim Benzema. Sasa habari zilizotoka August 3 kutoka kwa Wenger anashangazwa na taarifa hizo zinatoka wapi.

Benzema-BugattiMAIN

“Hakuna kinachotokea, kiukweli hakuna, sijui nani anaibua hizi taarifa, ni vyombo vya habari vya Hispania au Uingereza? Sijui”>>>Wenger

Baada ya kuwasajili Mesut Ozil na Alexis Sanchez misimu miwili iliyopita kwa dau ambalo sio kawaida kwa Wenger kununua mchezaji kwa kiasi hicho cha fedha, wengi walijua huenda atamsajili Benzema kutokana na mkurugenzi wa Arsenal Lord Harris kuthibitisha kuwa na kiasi cha fedha cha kutosha kumsajili mchezaji yoyote.

Hata hivyo kauli ya Wenger pekee haitoshi kwa vyombo vya habari kuamini kama kweli hana mpango na Karim Benzema kwani chochote kinaweza tokea.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments