Ad

Michezo

Bernard Morrison aachwa Dar E Salaam ✈️

on

Simba SC imetaja orodha ya majina ya wachezaji 24 watakaosafiri na timu kutoka Dar es Salaam kwenda Zimbabwe kuivaa FC Platnum 23/12/2020 mchezo wa round ya kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika.

Katika majina 24 yaliotajwa jina la staa wa Ghana Bernard Morrison ambaye alisajiliwa kutoka Yanga halipo katika kikosi hicho, haieleweki bado ni majeruhi au Simba SC imeendelea kutotaka kusafiri na lundo la wachezaji ambao haitowatumia.

Majina ya wachezaji 24 wa Simba SC waliosafiri kwenda Zimbabwe.

Hii ni mara ya pili kwa Bernard Morrison kuachwa katika safari ya timu, baada ya awali kuachwa katika mchezo wa Ligi Kuu timu ikielekea Mbeya kucheza dhidi ya Mbeya City alikuwa pamoja na Ajib lakini Simba imesafiri na Ajib safari hii.

Simba SC inaenda kucheza round ya kwanza dhidi ya FC Platnum baada ya kuitoa Plateau United ya Nigeria wakati FC Platnum wao wanafika hatua hiyo baada ya kuitoa Cosmo do Sol ya Msumbiji.

Soma na hizi

Tupia Comments