Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Hizi picha 2 za Beyonce akionekana kumgombeza Jay Z ndio zimechukua headlines kwa sana wiki hii!

on

bey argung

.

Wanasema hakuna uhusiano wa kimapenzi usio na milima na mabonde ndani yake, yani kuna wakati wa furaha na kuna wakati kunatokea dosari za hapa na pale na kutoelewana.

Jay Z na Beyonce ni miongoni mwa mastaa wa dunia ambao uhusiano wao wa kimapenzi umekua ukiangaliwa sana na hata kutolewa mifano kwa jinsi ulivyodumu kwa muda mrefu.

Wanasema hizi picha ni za ndani ya mgahawa wa Sushi Los Angeles Marekani walikua wakipata chakula lakini ikaonekana Beyonce ana hasira na anamgombeza Jay Z na kupigwa picha bila wao kujua.

Beyonce

Haikujulikana kilichomkasirisha Beyonce ila picha hizi walizopigwa bila kujua kama wanachukuliwa picha, zimewapa watu majibu mengi huku Beyonce akihusishwa zaidi kuanzisha noma hii sababu wakati wote Jay Z alikua mpole.

Beyonce ana umri wa miaka 33 sasa hivi wakati Jay Z anayo miaka 45.

Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments