Habari za Mastaa

Beyonce kwenye hii biashara ya chakula…

on

beyonce-jay-z-summer-holiday-pictures-snaps-europe-boat-yacht-blue-ivy-beach-vacation-baby-footprint-holding-hands-view-swimming-shots

Mwanamuziki nyota wa miondoko ya Pop ulimwenguni Beyonce amekuja na biashara mpya inayohusisha chakula ambacho kinashauriwa na madaktari.

Beyonce ameungana na daktari Marco Borges ambaye ni mwanasaikolojia wa mazoezi, wawili hawa wamekuja na mpango wa kufanya biashara ya kuwapelekea watu vyakula vya mboga ambavyo vinashauriwa na madaktari.

Aina ya chakula atakayouza Beyonce itakwenda sambamba na mpangilio maalum wa kula unaomsaidia mtu kupungua uzito na kubakia na uzito wa kawaida unaoshauriwa kiafya.

Biashara hii imetokana na diet ambayo Jay na Beyonce waliifanya kwa muda wa siku 22 ambapo walikuwa wanakula vyakula vya mboga pekee.

Jay na Beyonce.

Beyonce aliamua kuweka nguvu kwenye biashara hii baada ya kufuata mpangilio wa kula kwa siku 22 ambao alifuata pamoja na mumewe Jay Z mpango ambao unasaidia kupungua uzito na kurutubisha mwili.

Jay Z alizungumzia mpangilio mpya wa chakula ambao yeye na mkewe wataufuata siku moja kabla ya siku yake ya kuzaliwa ambapo aliandika kwenye mtandao wa Life and Times kuwa siku moja kabla ya kufikia siku yake ya kuzaliwa akiwa anatimiza miaka 44 ataanza mpangilio mpya wa chakula ambao utahusisha vyakula vya mboga pekee.

Hata hivyo bado haijafahamika lini biashara hii ya chakula ya Beyonce na Marco Borges itaingia sokoni.

Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments