Habari za Mastaa

Beyonce ku-perform tuzo za Oscar

on

Beyonce na Billie Eilish watatumbuiza wakati wa tuzo kubwa duniani katika filamu za Oscars Jumapili ijayo, lakini Van Morrison, ambaye amekuwa akipinga chanjo waziwazi hatahudhuria tamasha hilo, waandaaji wamesema jana.

Watatu hao wote wametajwa kuwania tuzo ya Wimbo Bora katika tamasha hilo la 94, sambamba na Lin-Manuel Miranda na Diane Warren, ambao nyimbo zao pia zitatuimbuizwa.

Wimbo wa mapenzi wa Beyonce wa “Be Alive” unaowania tuzo hiyo, uliandikwa kwa ajili ya filamu ya maisha ya mcheza tennis “King Richard,” ambayo ndani yake Will Smith anaigiza kama baba wa wacheza tennis nyota wa kike duniani, Serena na Venus Williams.

Soma na hizi

Tupia Comments