Habari za Mastaa

Unaambiwa Beyonce ataingiza fedha hizi kupitia Mrs Cater Show World Tour

on

Beyonce-Stage-600-x-450-2Beyonce anategemea kutengeneza kiasi cha dola millioni 200 mpaka kufikia wakati tour yake ya Mrs Carter Show itakapofikia tamati baadae mwaka huu, hii ni kwa mujibu wa kituo cha Televison cha MTV.
Tour hiyo, ambayp tayari ilishaingiza zaidi ya dola millioni 180 na kuweka rekodi ya ziara ya mwanamuziki wa kike iliyoingiza fedha nyingi katika mwaka 2013, inategemewa kuwa ziara yenye mafanikio zaidi kwenye historia ya muziki ya mama Blue Ivy. Pia ziara hiyo itamfanya kuwa mwanamziki mweusi aliyelipwa fedha nyingi katika historia ya muziki duniani.
Jambo la kuvutia zaidi ni kwamba Beyonce ambaye ni mke wa rapper Jay Z, ndio muongozaji na producer mkuu wa production nzima katika ziara hiyo, akiongoza bendi ya wanamuziki wote wa kike na madansa 8 wa kike huku wanaume wakiwa wawili tu madansa wa kifaransa ambao ni mapacha.
Ziara hii imeandaliwa na kampuni yake ya “Parkwood Entertainment”, ambayo pia inahusika na utayarishaji wa albam yake mpya na documentary yake ya “Life Is But A Dream.”

Tupia Comments