Ad

Habari za Mastaa

Beyonce anamchukuliaje Nicki Minaj kimuziki? Anamkubali ama…!? + (Video)

on

Baada ya kushirikiana kwenye ngoma ya ‘Feeling Myself‘, urafiki kati ya Nicki Minaj na Beyonce umezidi kuchukua sura mpya kadri siku zinavyokwenda. Wiki iliyopita Beyonce maarufu kama Queen Bey na Nicki Minaj maarufu kama The Queen of Rap waliziandika headlines baada ya wawili hao kushare stage moja na kutoa performance kali kwenye concert ya TIDAL X: 1020, Brooklyn jijini New York.

BEYNICKI2

Beyonce Knowles & Nicki Minaj.

Kwa jinsi mambo yanayoonekana sasa hivi, Beyonce ametokea kumkubali sana Nicki Minaj baada ya staa huyo wa muziki wa R&B kusikika kwenye ngoma ya Prince “Darling Nicki” akikubali kuwa Nicki Minaj ni ‘Queen wa Rap Music’… kwenye mazoezi ya wimbo huo Beyonce anasikika akiimba mistari hii…

>>> “I met this girl named Nicki, I guess you could say she was the rap queen, I met her in the studio lobby, but her booty looked bigger in the magazines… She said, Bey will you jump on this song of mine? How could I resist when I heard little Nicki rhyme?” <<< Beyonce Knowles.

Nicki Minaj hakuwa nyuma sana kushare na mashabiki wake hisia zake, kupitia page yake ya Twitter, Nicki Minaj alipost tweet iliyosema…

>>> “Bey has spoken ???????????????????????????????????? #RapQueen #QueenBey my #bayBey ???? Still have the #Tidal kisses to all my QUEENS.” <<< @NICKIMINAJ.

BEY

Wawili hao ambao sasa wamekuwa kama mabestie pia walishare na mashabiki wao kipande cha video ya mazoezi waliokuwa wanafanya kwa ajili ya maandalizi ya concert ya TIDAL, ambapo Beyonce anaonekana akiweka changamoto kubwa kwa Nicki kwenye mozoezi ya kucheza.

Unaweza ukaicheki video ya wawili hao hapa chini mtu wangu!

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments