Michezo

Virgil kamshinda Sterling, hiki ndio kikosi bora cha PFA 2019

on

Beki wa Liverpool Virgil van Dijk ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya PFA ya mchezaji bora wa mwaka 2019 akimzidi Raheem Sterling wa Man City ambaye alikuwa akiwania nae tuzo hiyo, tuzo hiyo ya chama cha wachezaji soka wakulipwa mwaka jana alishinda tena staa wa Liverpool Mohamed Salah hivyo tuzo imerudi tena Liverpool.

Kwa upande wa kikosi cha wachezaji bora wa PFA, mastaa wa Man City ndio wameonekana kutawala zaidi katika kikosi hicho, wakifuatiwa na wachezaji wa Liverpool na Man United wakifanikiwa kutoa mchezaji mmoja pekee ambaye ni Paul Pogba.

Liverpool wametoa jumla ya wacheza wanne ambao ni Virgil van Dijk, Sadio Mane, Robertson na Alexander Arnold wakati Man City wakiwa wametoa wachezaji wengi zaidi Sergio Aguero, Raheem Sterling, Benardo Silva, Fernandinho, Laporte na Ederson.

Simba na Yanga za kataa kuungana ili kucheza na Mabingwa mara 5 wa Europa League May 23

Soma na hizi

Tupia Comments