AyoTV

Michael Wambura sasa kumpeleka Mahakamani Wallace Karia wa TFF

on

Aliyekuwa Makamu wa Rais wa shirikisho la soka Tanzania TFF Michael Richard Wambura inaonekana bado hajakata tamaa na safari hii ametangaza kumburuza Mahakamani Rais wa TFF Wallace Karia.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri March 15 2018 Michael Richard Wambura alifungiwa maisha kujihusisha na soka na kamati ya maadili ya TFF kwa tuhuma za makosa matatu moja kupokea pesa za TFF isivyo halali, kugushi nyaraka na kushusha hadhi ya TFF.
 
Ila December 4 2018 zikiwa zimepita siku 265 toka adhabu hiyo itolewe Michael Wambura alienda TFFna hati ya Mahakama Kuu ya Tanzania ikiwa imetengua maamuzi hayo ya TFF kwa madai kuna baadhi ya taratibu zimekiukwa.
January 23 2019 TFF ilitangaza tena kuwa shirikisho la soka Ulimwenguni FIFA limetangaza kuridhia adhabu ya Micahel Richard Wambura kuwa afungiwe maisha kujihusisha na soka duniani kote.
Leo Wambura amejitokeza tena mbele ya waandishi wa habari na kusema kuwa Rais wa TFF au TFF kwa ujumla iliwasilisha adhabu ya Wambura FIFA pasipo kufuata utaratibu, haikuwa imesema kama Mahakama imetengua adhabu yake, haikuwa imesema kwamba amekata rufaa na badala yake imeeleza kuwa Wambura hakukata rufaa, hivyo ameamua kumpeleka Karia Mahakamani.


Msimamo wa Beno Kakolanya Yanga ndio huu, katuma tena barua

Soma na hizi

Tupia Comments