Premier Bet
TMDA Ad

AyoTV

VIDEO: Kwa tathmini hii ya Edo Kumwembe, Mashabiki wa Chelsea haina budi kuwa wavumilivu

on

Baada ya club ya Chelsea ya England ikiwa chini ya kocha wake mpya ambaye aliwahi kuwa nahodha wa timu hiyo Frank Lampard kucheza michezo miwili ya mwanzo pasipo uwepo wa ushindi, AyoTV ilimtafuta mchambuzi wa masuala ya soka Edo Kumwenbe aizungumzie tathmini ya kiwango cha Lampard.

“Frank bado hajapata formula ya ushindi lakini nilivyomuangalia ni bonge la kocha kwa maana ya aina ya mpira anavyofundisha Chelsea wapo vizuri sana katika kushambulia wepesi sana, unajua makocha wengi wa kizazi kipya wanamuiga Pep Guardiola ila sasa kuziba mashimo huku”>>> Edo Kumwembe

Hadi sasa Chelsea imefanikiwa kucheza michezo miwili ya Ligi Kuu ikipoteza mmoja na kutoka sare mmoja kwa kufungana 1-1 dhidi ya Leicester City, Chelsea ipo nafasi ya 15 katika msimamo wa Ligi Kuu ya England msimu wa 2019/20 ikiwa na point 1.

VIDEO: MWALIMU KASHASHA KATOA TATHMINI KWA YANGA HII DHIDI YA TOWNSHIP ROLLERS

Soma na hizi

Tupia Comments