Habari za Mastaa

Cardi B kuwaweka Rappers wa kike kwenye ngoma moja, vipi Nicki Minaj?

on

Kwa mujibu wa mtandao wa Rap Up umeripoti kuwa Rapper Cardi B yuko tayari kuwakusanya kwa pamoja rappers wote wa kike kwenye mdundo moja na kusema kuwa alikua na wazo hili kwa muda mrefu na kwa sasa kuhusu ishu ya majina itabaki kama siri moyoni mwake.

Kupitia kwenye mahojiano na Big Boy Tv, Cardi B alifunguka kuwa amepanga kufanya  hivyo kutokana na kushawishika kwa kiasi kikubwa na wimbo wa rapper mwenzake Lil Kim uliofanya vizuri mwaka 1997 “Not Tonight (Ladies Night Remix)” aliowashirikisha Missy Elliott, Lisa “Left Eye” Lopes, Da Brat, na Angie Martinez.

Cardi B alifunguka na kusema kuwa tayari majina yapo na wazo hilo ni zuri na ana imani kuwa lazima lifanyike lakini mpaka sasa ana mpango wa kuwashirikisha rappers wa kike wa nne na mmoja asiwe chini ya management yoyote.

VIDEO: ROSE NDAUKA KUHUSU KUTENGANA NA MZAZI MWENZAKE ‘NILICHOKA KILA MTU ATAVUNA ALICHOPANDA’

Soma na hizi

Tupia Comments