AyoTV

VIDEO: Kocha wa Taifa Stars katoa taarifa za majeruhi, Erasto akiwatoa hofu Watanzania

on

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars kwa sasa ipo nchini Sudan ikijiandaa kupambana na Sudan katika mchezo wao wa mwisho wa kuwania kufuzu fainali za CHAN 2020 nchini Cameroon, Taifa Stars inaingia katika mchezo huo ikiwa inahitaji ushindi wa kuanzia magoli 2-0 ili ifuzu kucheza fainali hizo.

Taifa Stars inahitaji ushindi huo kufuatia mchezo wao wa kwanza jijini Dar es Salaam walipteza 1-0, hivyo ni ushindi pekee ndio utawafanya wasonge mbele, kuelekea mchezo huo kaimu kocha mkuu wa Taifa Stars Etienne Ndairagije ameeleza kuwa wachezaji wake wapo kamili ila Tshabalala aliumia mchezo na Rwanda ila kwa sasa anaendelea vizuri, huku Erasto Nyoni akidhirisha kuwa

“Tumejaribu kuzoea hali ya hewa kwa haraka na hivyo mechi itakuwa usiku na sasa tunajiandaa kwenda mazoezi muda huu, Tshabalala aliumia Rwanda akacheza kidogo nikamtoa nikamwambia asicheze ile mechi apumzike tumefika hapa amefanya mazoezi kidogo sasa yupo sawa”>>> Etienne

AUDIO: SERGIO AGUERO WA MAN CITY AMEPATA AJALI

Soma na hizi

Tupia Comments