Habari za Mastaa

Rapper Drake ameisogeza project mpya yenye midundo 17

on

Fahamu kuwa leo August 2,2019 Rapper Drake ameileta project mpya kwa mashabiki zake inayofahamika kwa jina la ‘Care Package’ yenye jumla ya ngoma 17 ndani yake ikiwa inaelezwa kuwa ngoma hizo hazikuwahi kuwekwa kwenye mitandao ya kusikiliza na kupakua nyimbo.

Imeelezwa kuwa Drake amepata nafasi ya kuachia baadhi ya ngoma zake ambazo hazikuwahi kupata nafasi ya kuachiwa kabla akiwa studio huku ikiripotiwa kuwa ndani ya project hiyo kuna ngoma tokea mwaka 2010 ikiwemo ‘4PM in Calabas’, ‘Girls Love Beyonce’ na ‘Jodeci Freestyle’ akiwa amemshirikisha J.Cole.

Imeripotiwa kuwa ndani ya project hiyo ‘Care Package’ kuna ngoma ambazo hazikuachiwa rasmi ambapo ngoma kama ‘“Can I”  na “Dreams money can buy’ zilivuja hata hivyo baada ya Drake kuachia Album yake ya ‘Scorpio’ aliachia ngoma mbili Omerta na Money in the grave.

VIDEO: MAKOMANDO WAMEZUNGUMZA MAISHA YALIVYOKUWA LILIPOVUNJIKA KUNDI LAO “TUMERUDI UPYA”

Soma na hizi

Tupia Comments