Habari hii ilikamata hisia za wengi na hii ni baada ya bwana harusi wa Indonesia kutoweka siku ya arusi yake, baba yake ndipo alipochukua jukumu na kumwoa bibi harusi ili tu tukio hilo la gharama kubwa lisisitishwe.
Siku ambayo ilidhaniwa kuwa yenye furaha zaidi katika maisha ya mwanamke mmoja wa Kiindonesia iligeuka haraka kuwa jinamizi la kufedhehesha baada ya mtarajiwa kutoweka siku ya harusi yao.
Mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina moja pekee la SA na vyombo vya habari vya Indonesia, anatokea kijiji cha Jikotamo, Halmahera Kusini, na inasemekana alikuwa na uhusiano wa muda mrefu na bwana harusi lalakini, mnamo Agosti 29, siku ya harusi yao, mwanamume huyo alikimbia, akamwacha awaelezee wageni kwamba harusi ilikuwa imesitishwa.
jambo hilo lilionekana kuwa liisilowezekana na familia zote mbili, kwa kuwa maandalizi ya harusi yalikuwa yamegharimu pesa kidogo, na mahari ilikuwa tayari imetolewa , kwa hivyo baba ya bwana harusi aliingia na kumoa mkwewe kwa niaba ya mwanae.