Top Stories

Biden amwita Putin ‘mhalifu wa kivita’

on

Rais wa Marekani, Joe Biden, amemuita Rais wa Urusi, Vladimir Putin, mhalifu wa kivita, na kusema atamfungulia kesi ya uhalifu wa kivita.

“Uliona kile kilichotokea Bucha,” Biden alisema. Aliongeza kuwa Putin “ni mhalifu wa kivita”.

Biden pia alisema atatafuta vikwazo zaidi baada ya kuripotiwa ukatili nchini Ukraine, lakini maoni yake kwa waandishi wa habari hayakufika hadi kutaja vitendo hivyo kuwa ni mauaji ya halaiki.

“Tunapaswa kuendelea kuipatia Ukraine silaha wanazohitaji ili kuendeleza mapambano. Na inabidi tukusanye maelezo yote ili hii iwe kweli – kuwa na kesi ya uhalifu wa kivita,” Biden alisema, kulingana na matamshi yaliyotumwa na mtandao wa Associated Press.

 

Soma na hizi

Tupia Comments