Rais wa Marekani, Joe Biden ameagiza mashirika ya ujasusi ya nchi hiyo kuongeza nguvu katika kuchunguza chanzo cha Covid-19, ikiwemo nadharia ya kuwa virusi hivyo vilitengenezwa maabara.
Biden ameyataka mashirika yake ya kijasusi kukamilisha uchunguzi na kuripoti kwake ndani ya kipindi cha siku 90.
Covid-19 kwa mara ya kwanza iligundulika katika mji wa Uchina wa Wuhan mwishoni mwa mwaka 2019. Utata kuhusu asili ya virusi hivyo pado unaendelea kuongezeka.
Zaidi ya watu milioni 168 wamethibitishwa kupata maambukizi ya virusi hivyo kote duniani na takriban watu milioni 3.5 wameripotiwa kufa.