Top Stories

Biden ateua timu ya wanawake pekee kusimamia mawasiliano ya Ikulu

on

Rais Mteule wa Marekani, Joe Biden ameteua timu ya Wanawake pekee kusimamia Mawasiliano ya Ikulu (White House), hatua ambayo imetajwa kuwa ya kihistoria katika nchi hiyo.

Biden pamoja na Makamu wake, Kamala Harris ambao wataapishwa Januari 20, 2021 wamesema wamefanya uteuzi huo kama msisitizo kuwa wanajali utofauti katika jamii.

Miongoni mwa walioteuliwa ni pamoja na Jen Psaki ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ikulu katika utawala wa Barack Obama. Wengine ni Kate Bedingfield na Ashley Etienne.

Uteuzi huo hauhitaji kuthibitishwa na Seneti kama inavyokuwa kwa Mawaziri.

“HUYU MTOENI ASIRUDI” MKURUGENZI ALIEMDHARAU WAZIRI MKUU ATUMBULIWA PAPO HAPO

Soma na hizi

Tupia Comments