Habari za Mastaa

Duh! Kupiga ‘selfie’ na Justin Bieber itakubidi uwe na kiasi hiki cha mshiko!!

on

Zimepita siku chache tu toka Justin Bieber atangaze kuanza kwa tour yake ‘Purpose world tour ‘ mwanzoni wa mwaka 2016, tour itakayompeleka nchi 56 kwa ajili ya kuitangaza Album yake mpya, PURPOSE.

Licha ya ticket za tour hiyo kuuzwa bei ya juu, mitandao mingi Marekani imekuwa ikiripoti kasi ya ticket hizo kununuliwa huku wengine wakisema mwaka 2015 umeishia kuwa mwaka poa sana kwa Justin Bieber… Lakini kingine kikubwa cha kujua kuhusu tour hii ni package special ya VIP Selfie itakayopatikana kwenye tour ya Justin itakayoanza mwezi March mwaka 2016!

MILAN, ITALY - OCTOBER 25: Justin Bieber takes a selfie with fans at the MTV EMA's 2015 at the Mediolanum Forum on October 25, 2015 in Milan, Italy. (Photo by Vittorio Zunino Celotto/MTV 2015/Getty Images for MTV)

Kwa mujibu wa Altitude Tickets, package special ya VIP Selfie yani  ‘I’ll Show You VIP #Purpose Experience’ itauzwa kwa USD $925 ambayo ni sawa na milion 1,850,000, na watu watakaonunua package hiyo wataweza kupiga picha moja  tu (sio mbili wala tatu) ya pamoja (Group Selfie) na Justin Bieber na kushare na watu wao kwenye Instagram… cha kushangaza zaidi ni kwamba package hii ya ticket zimeshakwisha tayari, yani SOLD OUT!!

bibaselfie

Justin Bieber kwenye ‘Group Selfie’ na mashabiki wake.

Package nyingine zitakazopatikana kwenye tour ya Justin Bieber ni pamoja na ‘Where Are You Now’ VIP #Purpose Experience’ kwa $325 ambayo inagonga zaidi ya 600,000 za kitanzania, na ‘Ultimate #Purpose Experience’ kwa $2,000 ambayo kwa pesa ya nyumbani tunazungumzia mshiko wa milion 4 za Kitanzania!

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FBYOUTUBE

 

 

Soma na hizi

Tupia Comments