Habari za Mastaa

Unafahamu washiriki waliotupwa nje Big Brother? Hawa hapa

on

BBAAliyekuwa mwakilishi wa kutoka Kenya ndani ya jumba la Big Brother nchini Afrika Kusini, Sabina ametolewa katika jumba hilo.

Taarifa zilizowekwa katika ukurasa wa mtandao wa Standard Digital ya nchini Kenya zinasema, mwakilishi huyo ambaye pia ni mtangazaji wa televisheni amekuwa kivutio cha watazamaji wengi wa show ya Big Brother.

Sabina ametolewa ndani ya jumba hilo pamoja na wenzake ambao ni Lilian aliyekuwa mwakilishi kutoka Nigeria, pamoja na Esther ambaye pia alikuwa mwakilishi kutoka nchini Uganda.

Melvin Alusa, mwakilishi wa Kenya aliyesalia ndani ya jumba la Big Brother.

Melvin Alusa, mwakilishi pekee kutoka Kenya aliyesalia ndani ya jumba la Big Brother.

Melvin Alusa ambaye ni mdogo wa mwanamuziki Bien-Aime Baraza kutoka kundi la Sauti Sol, anasalia kuwa mwakilishi wa pekee aliyebakia ndani ya jumba la Big Brother akiwakilisha nchi ya Kenya, huku wakenya wengi wakiwa na tumaini la huenda Melvin akarudi na ushindi nyumbani kwa mwaka huu.

Kutolewa kwa washiriki hao kunafanya jumba hilo kubakiwa na idadi ya washiriki 21 tu, 8 kati yao ni washiriki wa jinsia ya kike na wa kiume 13.

Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments