Top Stories

Bila Kuogopa: Watumia jina la Janet Magufuli kujipatia Mil 15 (Video+)

on

Watu wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa kesi ya Uhujumu Uchumi ikiwemo kutumia jina la Janet Magufuli kupitia mtandao wa Facebook na kujipatia Sh.Mil 15 isivyo halali. Washtakiwa hao ni Masse Uledi (43) wa Kitunda Magore na mfanyabiashara Nkinda Shekalage (34), anayeishi Tegeta Wazo.

Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka matatu mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustina Mmbando ambayo ni kuchapisha taarifa za uongo kwenye mtandao, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kutakatisha fedha.

Soma na hizi

Tupia Comments