Asubuhi ya April 15 kabla ya mwili wa marehemu Muhidin Gurumo kusafirishwa kuelekea kijijini kwao Masaki Wilayani Kisarawe Makamo wa Rais Dkt Mohammed Gharib Bilal alihudhuria nyumbani kwa marehemu eneo la Tabata Kisukuru.
Nyumbani Tabata kwa marehemu kulikua na watu mbalimbali wakiwemo mastar wa Tanzania kama Jb kutoka Bongo Movie,Shamsa Ford,Dokta Cheni,Mb Dog,Ally Choki,Khadija miongoni mwa watu waliotoa michango yao ni pamoja na Mkurugenzi wa Vipindi na uzalishaji wa Clouds Fm Ruge Mutahaba ambaye alitoa basi mbili kwa ajili ya kusafirisha wafiwa kwenda Kijijini Masaki.