Shilingi bilioni 213 zimetumika kuboresha miundombinu mbalimbali katika manispaa ya temeke kupitia mradi wa uendeshaji jiji dar es salaam DMDP.
Kaimu Mratibu wa Mradi wa DMDP Temeke, Adelhard Kweyamba amesema walikuwa na miradi yenye thamani ya Sh. bilioni 213 iliyohusisha ujenzi wa Barabara, vituo vya Afya, viwanja vya michezo, mifereji, masoko na ujenzi wa vituo vya mabasi, mpaka sasa wameshafanya malipo ya Bilioni 197.
“Huu mradi tunategemea mpaka mwisho wa mwezi wa pili uweze kutumika na umegharimu kiasi cha Shilingi Milioni 998, ambapo utakuwa na kiwanja cha mpira wa Miguu, mpira wa pete, sehemu ya kuchezea ngumi sambamba na michezo ya watoto” Adelhard Kweyamba, Kaimu mratibu DMDP Temeke