Halmashauri ya Mafinga mji iliyopo mkoani Iringa imepitisha bajeti ya shilingi Billioni 27.9 kwa mwaka wa fedha 2024/2025 ambapo kati ya fedha hizo zaidi ya bilioni 5 zinatokana na mapato ya ndani ya halmashauri hiyo .
Hayo yamezungumzwa leo na afisa mipango na uratibu wa halmashauri ya mafinga mhi Peter Ngussa kwenye kikao cha baraza la madiwani lenye lengo la kupitisha rasimu ya bajeti ya mwaka huwo ambapo pia bilioni 5.5 ni ruzuku ya miradi ya maendeleo na nyingine bilioni 16.4 ni ruzuku ya uendashaji na mishahara kutoka serikali kuu
Hatahivyo kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya mafinga mji kiliangalia ripoti ya utekelezaji wa nusu mwaka ya ukusanyaji mapato ya ndani ya mwaka kwa mwaka wa fedha 2023/2024 na walifanikiwa kukusanya kiasi cha bilioni 2.8 sawa na asilimia 52.