Mix

Bill Clinton aingia kwenye kashfa nyingine ya kutoka nje ya ndoa yake

on

1Bill Clinton rais zamani wa Marekani aliwahi kuingia kwenye kashfa kubwa ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Monica Lewinsky ambaye alikuwa na miaka 22 kipindi hicho akifanya kazi kama intern ndani ya White house.

Skendo hiyo ilivyoendelea kuwa kubwa ilimpelekea hadi Bill Clinton kukanusha waziwazi kwa kusema kwamba hakuwa na mahusiano ya kimapenzi na miss Lewinsky kama ilivyokuwa inasemekana.

moni

Monica Lewinsky

Kitu kipya ni kwamba mtandao mmoja huko Marekani ambao hutoa habari za kuaminika, umetoa habari na kusema kwamba Bill Clinton alicheza faulo nje ya ndoa yake na actress/model Elizabeth Hurley.

elizabeth-hurley-estee-lauder-and-the-estee-lauder-companies-breast-cancer-awareness-campaign-spokesmodel-body-1335640949

Elizabeth Hurley

Ripoti ya mtandao huo unasema kwamba Bill Clinton alikuwa na uhusiano na model huyo kwa muda wa zaidi ya mwaka mzima bila mke wake Hillary Clinton kujua.

Ripoti hizi kama zikithibishwa ukweli ndani yake, zinaweza kuharibu harakati za Hillary Clinton ambaye anajiandaa kugombania urais mwaka 2016.

Hata hivyo mwanamitindo/muigizaji Elizabeth Hurley hakukaa kimya na kuandika tweet akikanusha taarifa hiyo na kusema kila kitu ameshawakabidhi wanasheria wake washughulikie hili swala.
1a

Tupia Comments