Ni Desemba 19, 2022 Katibu Mkuu Utumishi Dr.Lauren Ndumbaro amewataka watumishi wa Tira hapa nchini kuhakikisha wanatoa elimu kwa wananchi kwa lugha rahisi ili kuwezesha Jamii kufahamu zaidi umuhimu wa bima hapa nchini.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa tatu wa baraza la Wafanyakazi wa mamlaka ya usimamizi wa bima (TIRA) Mkoani Tanga Katibu Mkuu utumishi Dr.Lauren amesema kuwa ni wajibu sasa wa Watumishi wa bima kuwa wabunifu katika utoaji wa Elimu ili kuhamasisha watu wengi kujiunga ili kusaidia Jamii lakini pia kuongeza mapato ya nchi.
”Ni wakati sasa kufikiria kuendesha kazi zenu kidigitali ili kuwezesha mambo mengine zaidi kwenda kwa urahisi zaidi kwani Mhe.Rais Dr.Samia suluhu Hassan nia yake kubwa ni kuona tasisi nyingi za kiserikali zikitekeleza majukumu yao kidigitali zaidia” Alisema dr Ndumbaro
Aidha dr.Ndumbaro amewataka watumishi kuweka usiri zaidi katika kutoa huduma ili kuwepo usiri baina na mtumishi na mteja Sambamba na kuzingatia uzalendo na kufanya kazi kwa juhudi na maarifa.
Hata hivyo kamishina wa Tanzania Dr.Baghayo Saqware amebainisha changamoto mbalimbali wanazo kutana nazo wakati wa utekelezaji wa majukumu yao kwenye sekta ya bina ambayo ni kutokuwepo kwa sera ya bima hapa nchini pamoja na kutokuwepo kwa bodi ya taifa ya bina na hivyo kupelekea mambo mengi ya kiutumishi kukwama.