Msemaji wa Yanga amesema Jumatano ya tarehe 15 ni siku ya Mwananchi, siku ya Mwanayanga, siku maalum… ikiwa ni siku ambayo Club hiyo itakwenda kutengeneza historia nyingine kama itapata matokeo yanayohitajika huku akisisitiza kwamba kushinda ubingwa mara 28 sio kitu rahisirahisi.
“Hadi sasa sisi ndio Bingwa wa muda wote kwa Tanzania, sipendi sana kutumia neno Bingwa wa Kihistoria, napenda kutumia Bingwa wa muda wote lina heshima hilo jina kama vile Manchester United alivyokuwa Bingwa wa muda wote wa Uingereza au Real Madrid Bingwa wa muda wote wa Ulaya basi Tanzania Bingwa wa muda wote ni Yanga na tuna mataji 27 Mungu akitujalia tunakwenda kupata taji la 28 msimu huu na tutafurahi sana tukilipata jumatano”