Top Stories

Binti wa kazi amuua mtoto wa boss mwenye miaka minne, vurugu zaibuka (video+)

on

Msichana wa kazi za ndani mwenye umri wa miaka 13 Mkazi wa kata ya Moshono jijini Arusha anadaiwa kumuua kwa kipigo Mtoto wa Boss wake mwenye umri wa miaka minne aitwae Natalia Essau.

Janeth Temba ambaye ni Mama wa Marehemu amesema alipigiwa simu na Mfanyakazi wake na kuambiwa anaumwa ambapo alipofika alimkuta Mtoto wake ameshafariki na alipokaguliwa alikutwa akiwa na majeraha sehemu mbalimbali ikiwemo kichwani.

“Nilipigiwa simu na Msichana wa kazi akaniambia Mtoto wangu anaumwa, anaharisha…. nikamuuliza sasa hivi anaendeleaje? akaniambia nimempa dawa amelala, nikamwambia akiamka unipe niongee nae lakini zikapita kama dakika 10 akanipigia tena”

“Akaniambia Dada leo usichelewe amezidiwa, ndio nikawahi kuja huku nikakuta Mtoto wangu ameshafariki tayari amekua wa baridi, Majirani wakampeleka Hospitali ile kukaguliwa wakaambiwa ana majeraha yaliyovimbia damu kuanzia kichwani, mwilini wakasema ndio kitu kilichosababisha kifo chake” ——— asema Janeth Temba, Mama wa Marehemu.

Jeshi la Polisi limethibitisha kumshikilia Msichana huyo wa kazi za ndani na kusema wanaendelea na upelelezi zaidi kuhusiana na tukio hili.

Tupia Comments